Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka watumishi katika halmashauri za mkoa huo kufanya kazi kwa kujituma na kuacha kukaa maofisini kusubiri mishahara.

Makonda ametoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 10 katika mkoa huo iliyoanza jana katika wilaya hiyo.

Amesema asilimia 80 ya watumishi hao hawapendi kufanya kazi kwa kujituma jambo linalosababisha wananchi kukosa huduma stahiki.

Aidha aliwataka maofisa biashara kuwa na mahusiano mazuri na wafanyabiashara na kuwa washauri na namna ya kujenga biashara zao jambo ambalo litaleta hamasa ya ulipaji kodi kwa wafanyabiashara hao.

Pia amewataka watumishi hao kuepuka kushiriki vitendo vya rushwa wakati wa ulipaji wa fidia badala yake wafanye kazi kwa haki na usawa lengo likiwa ni kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.

Makonda amesema uchimbaji huo umesababisha uharibifu wa nyumba nyingi ambazo zimebaki zikining’inia na kuwa hatari kwa wakazi wa nyumba hizo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *