Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka watendaji wote wa Kata kuwa na taarifa zote za miradi ya maendeleo vinginevyo atawachukulia hatua stahiki.

 Makonda amemtolea mfano Mkuu wa Wilaya Bungo, Humphrey Polepole kwa kuwa na taarifa mbalimbali kuhusu miradi ya maendeo na kuwaomba waige kutoka kwake.

Pia Makonda amemuagiza RPC Mkoa wa kipolisi Kinondoni Suzan Kaganda kwa kushirikiana na TAKUKURU kumshikilia na kumfanyia uchunguzi aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Msigani mtaa wa Temboni, Neema Kalumbe ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa Kata ya Makongo kujibu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa Barabara ya kutokea Msuguri na Msingwa ambao ulitengewa milioni 17 na hakuna barabara iliyojengwa.

Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka mwenyekiti wa wa Mtaa wa Temboni, Msigani Israel Mushi kutofanya kazi kwa upendeleo kwani kuna Mkazi aliyefahamika kwa jina la Maureen Gomba ambaye amelalamikia kuwa mwenyekiti huyo amekuwa akigawa vizimba kwa watu anaowafahamu.

RC Makonda amewatoa hofu wakazi wa maeneo hayo kuhusu huduma ya maji na kwani kwasasa mradi huo upo chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASCO, huku Mkuu wa Wilaya hiyo akihaidi kukutana na wananchi hao ili kumaliza kero hiyo kabisa ifikapo Desemba 21

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *