Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul, Makonda amewataka wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wasiingie katika matukio ya kihalifu yanayoendelea katika jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa huyo amesema hayo katika uzinduzi wa madarasa nane ya Shule ya Msingi Mbande iliyoko wilayani Temeke jijini Dar es Salaam kwenye muendelezo wa ziara yake.

Makonda amesema mtoto yeyote aliye chini ya umri wa miaka 17 atakaye kamatwa kwa tuhuma za uhalifu, na wazazi wa mtoto huyo atakamatwa.

RC Makonda amewataka wazazi hao kuwahimiza watoto wao kusoma pamoja na kufuatilia maendeleo yao ya kila siku.

Mkuu wa mkoa yupo ziarani katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam akisikiliza kero za wananchi wa jiji hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *