Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ametoa siku 14 kwa wakuu wa wilaya za mkoa huo kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wadogo (Machinga) wanafanya biashara kwenye maeneo yao waliopangiwa.

Makonda amesema kuwa kauli ya Rais Magufuli ya kwamba wamachinga wasibugudhiwe isitumike vibaya kwani hata wao wamachinga wanatakiwa wasiwabugudhi wananchi wengine kwa kufanya biashara mbele ya maduka na barabarani.

Mkuu wa mkoa huyo ameongeza kwamba wamachinga wanajitafutia ridhiki lakini hawapaswi kuvunja sheria ya kufanya biashara katika maeneo ambayo siyo rasmi.

Makonda ameendelea kwa kusema kuwa barabara zimejengwa kwa gharama kubwa hivyo haziwezi kbadilishwa matumizi na kuwa sehemu ya machinga kupanga na kuuzia bidhaa zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *