Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 10 kufungwa kwa mfumo wa camera wa CCTV kwa ajili ya kubaini matukio ya kiharifu jijini Dar es Salaam.

Makonda amesema hayo wakati wa mkutano  na wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ufungaji wa mfumo wa ufuatialiji wa makosa mbalimbali yanayotokea hapa Dar ikiwemo ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani zinazofanywa na baadhi ya madereva wa magari.

Mkuu wa mkoa huyo ametoa siku kumi kwa tume atakayoiunda ije na majibu ya suluhisho la namna mfumo huo utakavyoweza kufanya kazi,ameeza kwamba.

Makonda amesema kuwa “wako wataam walishakwenda mpaka China na serikali kugharimia safari na mafunzo tangu serikali ya awamu ya nne na akaagiza CAMERA zifungwe lakini mpaka leo hakuna lolote”

Amesema kuwa ,”Sasa mimi siendi nchi yoyote nipo hapahapa Dar es Salaam na nitahakikisha CAMERA zitafungwa”.

Mfumo huo ni Tanzania Tracking Technology of Security Monitoring System. Mfumo huu waweza kusaidia kutambua aina ya gari,jina la driver na hata kuweza kuzima/switch off gari iliyoibiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *