Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya askari wa usalama barabarani zenye thamani ya shilingi smillion 40 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.

Hatua hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza Misafara ya viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki hizo.

Makonda amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 600, Pikipiki 200 Computer , na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.

Aidha Makonda amemuagiza aliekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.

Agizo hilo limekuja baada ya Makonda kubaini uwepo wa Askari wanaowalinda Wafanyabiashara wa Dawa za kulevya, Askari wa Uwanja wa ndege wanaoshirikiana na Raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na Askari wanawabambikia kesi wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.

Amesema hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda kuwanyanyasa Wananchi na kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi na kufanya Wananchi kushindwa kutoa ushirikiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *