Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kutengwa sehemu maalumu kwaajili ya kuwazika viongozi mbalimbali waliofanya mambo muhimu katika nchi.

Makonda ametoa ombi hilo wakati akizungumza katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam katika shughuli za kuagwa marehemu Samuel Sitta.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema “Na ombi langu mheshimiwa rais ninalolileta kwako, ikiwezekana kama kutakuwa na nafasi tunao viongozi wengi sana akiwepo Baba wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere, wakina Olinge Sokoine siku zinavyokwenda unafikia wakati historia zao zinapotea.

Pia amesema Tulikubali makao makuu ya nchi yetu yawe Dodoma tuwe na eneo maalum na mahususi kwaajili ya kutenga na kuwahifadhi na kuwazika viongozi wetu waliofanya jambo kubwa katika historia ya maisha yetu ili iwe kumbukumbu kwa kizazi na kizazi kitakwenda na kusoma historia zao na kujua nini walifanya katika taifa letu,” alisema Makonda.

Vile vile mkuu wa mkoa hyo ametolea mfano nchi kama Ufaransa kwa kusema “Kama Ufaransa, yapo makaburi ya viongozi na wananchi waliofanya makubwa ambayo yamebaki kama sehemu ya kumbukumbu”.

Pia aliongeza kwa kusema “Kwahiyo nilikuwa naomba pale Dodoma tutenge ardhi sehemu ambayo itabaki kama kumbukumbu ya kuwahifadhi viongozi wetu na Mungu ikimpendeza tutaubeba mwili wa mpendwa wetu Mwalimu Julius Kambarage nyerere kuuleta Dodoma kama sehemu ya watu kujifunza historia ya nchi yetu,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *