Mkuu wa Mkoa wa Da es Salaam, Paul Makonda amemkabidhi Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na kupambana dawa za kulevyaorodha ya majina 97 wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya

Orodha hiyo aliyokabidhiwa Kamishna Rogers William Sianga ni ya awamu ya tatu katika muendelezo huo wa watuhumiwa wa dawa za kulevya katika jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam, Paul Makonda akimkabidhi Kamishna wa kupambana na madawa ya kulevya, Rogers William Sianga majina 97 ya wahusika wa dawa za kulevya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimkabidhi Kamishna wa kupambana na madawa ya kulevya, Rogers William Sianga majina 97 ya wahusika wa dawa za kulevya.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mwalimu Jilius Nyerere uliopo Posta jijini Dar es Salaam.

Mkutano umehudhuriwa na viongozi wengine wengi wa mkoa, ambapo kwa pamoja wameendelea kusisitiza kwamba vita hiyo ya madawa ya kulevya ni endelevu na wataendelea kupambana kuhakikisha madawa ya kulevya yanaisha Dar es Salaam na wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *