Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemaliza tofauti yake iliyokuwepo kati yake na vyombo vya habari nchini.

Tofauti hizo zimemalizwa leo mbele ya waandishi wa habari ambapo mkuu wa mkoa alikuwepo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari pamoja na mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba.

Makonda alifungiwa na Jukwaa la wahariri nchini (TEF) baada ya kuvamia ofisi za clouds Media akiwa na askari huku akiwatisha baadhi ya waandishi na watangazaji wa kituo hiko cha TV.

Kwa upande wa TEF, wamesema kuwa wameamua kumaliza mgogoro huo na mkuu wa mkoa kutokana na maslai na maendeleo wa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Jukwaa hilo limesema kuwa kwasasa limeruhusu kuandikwa kwa habari za mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuanzia sasa.

Siku chache zilizopita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliwapatanisha, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Ruge Mutahaba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *