Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, Paul Makonda amesema kuwa atahakikisha sekta ya afya ina kuwa bora ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.

Makonda amesema hayo wakati akikagua wodi ya akina mama katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala Jijini Dar es salaam.

Katika ukaguzi huo Makonda amesema kuwa kukamilika kwa wodi hiyo kutasaidia kuondoa msongamano mkubwa uliokuwepo kipindi cha nyuma hivyo amewaasa wahusika kutunza wodi hiyo.

Ameongeza kwa kusema kuwa kuwa katika idara ambayo anaamini kuwa itafanya vizuri katika mkoa wa ni sekta ya afya kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakijitolea kusaidia katika sekta hiyo.

Pia amewashukuru watu wote waliojitolea kuweza kuchangia hivyo amewaasa wananchi kujitokeza kuungana na Serikali katika kuujenga mkoa wa Dar es salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *