Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa atashirikiana na wasanii nchini kwa ajili ya kumtafuta Roma aliyetekwa juzi usiku.

RC Makonda amesema hayo leo alipokuwa anaongea na baadhi ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

Makonda amesema kwa upande wa Serikali amewaagiza maofisa wa usalama kwa ajili ya kufanya upepelezi kuhakisha Roma na wenzake wanapatikana.

Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro ameagiza maofisa wa upelelezi ambao watashiriki kumtafuta alipo Roma kutokana na kutokuwepo katika kituo chochote cha Polisi.

Makonda amewaambia wasanii waungane kutokana na suala hilo huku akisisitiza kushirikiana na wasanii hao kwa ajili ya kujua alipo Roma na wenzake ili waliofanya hilo waweze kushughulikiwa.

Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa kabla ya Jumapili atahakikisha Roma na wenzake watakuwa wameshapatikani kutokana na kazi iliyoanzwa kufanywa na Jeshi la Polisi chini ya Kamanda Sirro.

Pia Makonda amewataka wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuacha kuongea habari zisizokuwa na ukweli kuhusu suala la kutekwa kwa wasanii hao na kama kuna mtu atakuwa na taarifa anatakiwa kutoa taarifa hizo kituo cha Polisi cha Oysterbay.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *