Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amefunguka na kusema kuwa anafurahishwa na ushindani wa kimuziki kati ya Diamond Platnumz na Alikiba.

Makonda amesema kuwa ushindani huo unachangamsha muziki hapa lakini ushindanbi huo usiendele mbali kufukia kuvunja sheria na maadili ya nchi.

Makonda ambaye ni rafiki mkubwa wa wasanii nchini amesema kuwa anapenda sana anavyowaona vijana hao wakishindana na ushindani wao unafanya muziki ukue kwa kufanya kazi nzuri na kuitangaza nchi.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Makonda ameandika “Tofauti zenu mimi nazipenda, kwani zinaleta ushindani mzuri kwenye mziki“.

Pia Makonda ameongeza kwa kuandika skuwa “Ila naomba mzingatie sheria na Utamaduni wetu..“.

Wasanii hao kwasasa wanatamba na nyimbo zao, Alikiba akitamba na wimbo wake ‘Seduce Me’ huku Diaomond akitamba na wimbo wake ‘Zilipendwa’ akiwa na wasanii wake wa WCB.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *