Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana amekutana na kufanya mazungumzo na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Lazaro Mambosasa.

Kamanda Mambosasa ameripoti kwa Mkuu wa Mkoa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalam wa mkoa baada ya kuteuliwa hivi karibuni na IGP, Simon Sirro.

Kabla ya uteuzi huo Kamanda Mambosasa alikuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma ambapo sasa amekuwa kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam akichukua nafasi ya Simon Sirro aliyeteuliwa kwa IGP.

Katika Mazungumzo hayo wamejadili hali ya Usalama Jijini Dar es Salaam na namna ya kuendeleza yale ambayo yaliachwa na IGP Simon Sirro wakati akiwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Pia kamanda huyo jana amefanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa jiji la Dar es Salaam baada ya kuteuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *