Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo ametembelea eneo la bomoabomoa Tuangoma katika Wilaya ya Temeke na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ishu ya bomoabomoa katika eneo hilo.

Akiwa katika eneo hilo RC Makonda amewatoa wasiwasi wananchi ambao wamekuwa na hofu baada ya kuambiwa watabomolewa nyumba zao lakini akawaambia kuwa hakuna atakayewabomolea nyumba zao.

Amesema kuwa ”Nawaomba tujiepushe na sehemu hatarishi, kila kinachofanywa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaokoa wananchi. Hakuna mtu atakayewabomolea nyumba zenu, hata Rais aliniambia hamkumchagua ili awabomolee nyumba zenu.

Pia Maonda amesema kuwa “Tulikubaliana na Rais kuwa nyinyi mjiepushe kujenga kiholela na kwenye maeneo hatarishi na mfuate utaratibu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *