Kiungo wa zamani wa Real Madrid na Chelsea, Claudio Makelele ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Swansea City chini ya kocha Paul Clement aliyechukua mikoba ya Bob Bradrey aliyetimuliwa.

Makelele mwenye umri wa miaka 43 amesaini mkatabwa wa miezi sita na klabu hiyo ambapo atafanya kazi mpaka mwisho wa msimu huu.

Kiungo huyo anajiunga tena na kocha Paul Clement ambaye alifanya kazi naye akiwa mchezaji wa Chelsea kutoka mwaka 2007-2008 pamoja na akiwa kocha wa PSG chini ya meneja Carlo Ancelotti.

Baada ya kukamilika kwa uteuzi huo Makerere amesema kuwa ”Nimefurahi sana kuwa hapa na kufanya kazi na Swansea, Paul ni mshauri wangu . Amenifunza mengi wakati nilipofanya kazi naye.Niliposikia kwamba alirudi katika ligi ya Uingereza nilimpigia simu na kumuuliza iwapo naweza kumsaidia klabu ya Swansea”.

Makelele anatarajia kuwa kwenye benchi la klabu ya Swansea kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Arsenal mwisho wa wiki katika uwanja wa Liberty Stadium.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *