Makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yamechomwa moto katika mji mkuu wa Kinshasa huku mili miwili ilioungua ikipatikana ndani yake.

Mashambulio hayo yanajiri kufuatia makabiliano ya siku ya Jumatatu kati ya maafisa wa polisi na wafuasi wa upinzani wanaomtaka rais Joseph Kabila kujiuzulu ifikiapo mwezi Disemba.

Ofisi ya chama kikuu cha upinzani UPDS ni miongoni mwa zile zilizochomwa mjini Kinshasa.

Upinzani umemuonya Kabila kwamba atakuwa akifanya ”uhaini” kwa kuchelewesha uchaguzi.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba ,lakini upinzani unahofia kwamba rais anataka kuuahirisha kwa lengo la kutaka kusalia madarakani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *