Makamu wa rais nchini Gambia, Isatou Njie-Saidy amejiuzulu saa chache kabla ya muda wake wa kuongoza kumalizika.

Waziri wa mazingiura na elimu ya juu pia alijiuzulu,ikiwa ni msururu wa mawazuri kumtoroka Jammeh kufuatia hatua yake ya kukataa kujiuzulu baada ya zaidi ya miongo miwili afisini.

Wakati huohuo wakili wa rais Yahya Jammeh ametorokea nchini Senegal baada ya kumuandikia barua rais Jammeh akimtaka kuachilia mamlaka..

Bw Gomez alimwakilisha Jammeh katika harakati za kufutilia mbali ushindi wa kiongozi wa upinzani Adama Barrow katika uchaguzi wa tarehe mosi Disemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *