Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku tatu mkoani Mara.

Akiwa mkoani humo Makamu wa Rais atatembelea Wilaya ya Tarime katika kituo cha Afya cha Nyamwanga kinachojengwa na wananchi kwa msaada wa mgodi wa Acacia North Mara.

Katika ziara hiyo makamu wa Rais atatembelea katika bonde la mto Mara kunakokusudiwa kuanza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari mkoani humo.

Pia makamu wa Rais atatembelea wilya ya Serengeti ambapo ataweka jiwe la msingi katika  hospitali ya wilaya hiyo baada ya kuhudhuria.

Makamu wa Rais Pia atatembelea katika wilaya ya Musoma ambapo ataweka jiwe la Msingi kwenye Barabara KM 9.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami katika manispaa ya Musoma.

Ziara hiyo inatarajiwa kuanza Juni 5 mwaka huu katika mkoa huo wa Mara ikiwa ni ziara yake ya kwanza ndani ya mkoa huo toka awe makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *