Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezitaka Taasisi za fedha kuwawezesha wajasiriamali ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Mama Samia amengumza hayo mara baada ya kutembelea maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Dar es Salaam Sabasaba.

“Serikali itaendelea kuhamasisha taasisi za fedha hapa nchini ili ziendelee kuwawezesha wajasiriamali na hatimaye kwa pamoja tufikie azma ya Tanzania ya Viwanda,”alisema Mama Samia.

“Kwa ujumla niseme tu maonesho ni mazuri na tumeongeza muda ili watanzania wengi zaidi waje watembelee na kujionea bidhaa mbalimbali na huduma zinazotolewa “ Alisisitiza Mhe. Samia

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage alisema serikali imejipanga kuhakikisha kuwa viwanda vyote walivyopewa wawekezaji vinaendelezwa na kuzalisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *