Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameitaka TAKUKURU kuongeza kasi ya kuwabaini na kuwachukuliaa hatua za kisheria wahalifu wa vitendo vya rushwa nchini.

Makamu wa Rais ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu na uzinduzi wa Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

Samia amesema kuwa mapambano dhidi ya rushwa hayajaelekezwa upande wa watumishi wa Serikali pekee bali pia kwa wafanyabiashara pamoja na asasi za kiraia.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa Serikali itaendelea kutambua mchango wa taasisi za uwajibikaji na utawala Bora katika jitihada zao za kuimarisha misingi ya Utawala bora, uwazi, uadilifu na uwajibikaji.

Vile vile Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika taasisi hizo ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora za ukaguzi zenye kuleta tija kwa wananchi na hivyo kuimarisha uwajibikaji na thamani ya fedha kwenye makusanyo na matumizi ya rasilimali za umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *