Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amezindua fursa za ajira kati ya Watanzania na Wachina.

Zoezi la uzindui huo umefanyia leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi kibao akiwemo Balozi wa China nchi Tanzania.

Chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia taasisi ya Confucius, pamoja na ubalozi wa China na Chinese Chamber of Commerce, ndiyo waliokuwa waandaaji wa tukio hilo la kutafuta fursa za ajira kwa vijana wanaohitimu masomo yao.

Noble Victoria Centre itawasaidia vijana kupata ajira, hususan kwenye sekta ya sayansi na teknolojia kwa kuongeza ukubwa wa soko la ajira kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *