Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo ataongoza wakazi wa Arusha kuaga miili ya wanafunzi waliofariki katika ajali ya gari Arusha.

Serikali imegharamia sanda  na majeneza kwa wanafunzi wa shule Lucky Vicent waliopoteza maisha jana kwenye ajali.

Akitoa taarifa hiyo lMeya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro,  amesema taarifa za awali zinaonyesha tayari serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda za kuhifadhia miili ya marehemu.

Miili hiyo inatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo mbali na makamo wa Rais viongozi wengine watahudhuria mazihi hayo.

Aidha Lazaro amesema viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vincent  kwa ajili ya kikao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *