Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua makumbusho ya Olduvai Gorge, ambako ni chimbuko la historia ya binadamu.

Katika uzinduzi huo, Makamo wa Rais amesema kuwa makumbusho hayo ni kielelezo cha maisha na ustaarabu wa binadamu ambao unaelezea maisha ya vizazi vilivyopita.

Amesema ujenzi wa makumbusho hayo utasaidia kuvutia watalii na wanasayansi wa masuala ya mambo kale duniani.

Samia amesema eneo la Ngorongoro lina historia kubwa ya maisha ya zamadamu ikibainika miaka 3 milioni iliyopita walikuwepo walioishi kwa kutembelea miguu miwili.

Amesema eneo la Ngorongoro kumebainika miaka 2.7 milioni iliyopita binadamu walianza kutumia zana za mawe katika kula nyama na kuwinda.

Makamu wa Rais ameishukuru Jumuiya ya Ulaya kwa kutoa fedha kugharimia ujenzi wa makumbusho hayo na miundombinu yake.

Pia Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuwa na mkakati wa kutangaza makumbusho hayo ndani na nje ya nchi ili kuvutia zaidi watalii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *