Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshawasili mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya shughuli za serikali.

Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro,  Anna Mghwira pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Makamu wa rais anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Kilimanjaro.

Maadhimisho hayo yatafanyika kesho Jumatatu katika viwanja vya Mashujaa Moshi ikiwa na kauli mbiu isemayo “Zuia ajali tii sheria okoa maisha.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *