Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemtaka Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa kuhakikisha kanda yake inatokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Samia ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo.

Mama Samia alisema serikali inaendelea kutekeleza Mpango mkakati wake wa miaka mitano wa kutokomeza ukatili wa jinsia ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto unapungua kwa asilimia 50.

Pia Mama Samia alisema serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwakomboa wanawake ikiwemo kufufua Benki ya Maendeleo ya Wanawake nchini (TWB).

Aidha, Mama Samia aliwataka wanaume kutowanyanyasa wanawake kwa kuachana na mila na desturi potofu zinazokandamiza haki za wanawake na jinsia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *