Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amehudhuria mkutano wa jopo la Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa la kuwawezesha wanawake kiuchumi kama mmoja wa mjumbe wa jopo hilo.

Mkutano huo umefanyika katika nchi za Falme za Kiarabu na ufunguzi rasmi ulifunguliwa na mrithi wa mtawala wa Dubai Mtukufu Shekh Hamdan Bin Mohamed Bin Rashid Al Maktoum pamoja na viongozi wa Serikali ya Falme za kiarabu.

Lengo la mkutano huo ni kupitia ripoti ya jopo hilo iliyowasilishwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa Septemba mwaka jana.

Wajumbe wa Jopo hilo walipata fursa la kujadili changamoto mbali mbali zinazomkabili mwanamke pamoja na kubadilshana uzoefua na kutoa mapendekezo yatakayotoa matokeo chanya yatakayomuinua mwanamke kiuchumi.

Katika mkutano huo Makamo wa Rais amesema kuwa pamoja na kila Bara kuwa na changamoto zake bado kuna umuhimu wa dunia kuhakikisha inaweka misingi madhubuti ya kuinua wanawake kiuchumi hasa kwa wanawake wa ngazi za chini ambao wengi wanaishi vijijini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *