Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo anatarajia kuanza ziara ya siku 4 mkoani Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Mkoa wa Dodoma imesema akiwa mkoani Dodoma, Makamu wa Rais atakagua shughuli mbalimbali za maandalizi ya kupokea ujio wa serikali mkoani Dodoma.

Aidha Makamu wa Rais atakagua ujenzi wa majengo ya serikali, miradi ya usafi wa mazingira kwa kutembelea dampo la kisasa lililopo Chidaye nje kidogo ya mji wa Dodoma na kufanya mkutano na makundi mbalimbali yanayoendesha shughuli zenye uhusiano na mazingira.

Ofisa habari wa Mkoa wa Dodoma, Jeremia Mwakyoma amesema Makamu wa Rais kesho kutwa akiwa mkoani hapa anatarajiwa kufungua mkutano wa mwaka wa waganga wakuu wa mikoa, wilaya na waganga wafawidhi wa hospitali Tanzania Bara.

Aidha amesema kwamba maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mapokezi ya Makamu wa Rais na ziara yake yamekamilika na kuwaomba wananchi na wadau wote wa maeneo yatakayohusika na ziara hiyo kushiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *