Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kuwa Serikali imeunda kikosi kazi cha taifa kwa ajili ya kufuatilia utengenezaji wa pombe aina ya viroba.

Kikosi kazi hicho, mbali na kufuatilia pia kitakuwa na jukumu la kufanya ukaguzi na kitajumuisha Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) , Uhamiaji na Polisi.

Amesema “Serikali imeunda kikosi kazi maalum cha kitaifa kwaajili ya kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa hatua hizi tulizozitangaza leo, kikosi hicho kinajumuisha watu kutoka ofisi ya Makamu wa rais, wizara ya mambo ya ndani ya nchi, wizara ya fedha na mipango,.

Pia wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, wizara ya afya, baraza la taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira, mamlaka ya chakula na dawa, TBS,TRA, idara ya uhamiaji na jeshi la polisi, doria za ukaguzi kwaajili ya utekelezaji zitaanza wakati wowote kuanzia sasa.”

Waziri Makamba amesema kuwa “Mtu yeyote atakayekamatwa katika doria hizo ambaye amekiuka masharti kwa masharti tuliyotangaza siku ya leo na hatua tulizotangaza siku ya leo kuanzia tarehe aliyoitangaza Waziri mkuu kuanzia tarehe 1 mwezi Machi atachukuliwa hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaokiuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *