Mkuu wa mkoani wa Mbeya, Amosi Makalla amesema kuwa uchumi wa wananchi unaweza kukua kwa haraka endapo baadhi ya watumishi wa umma ambao si waadilifu wataepuka vitendo vya rushwa.

Makalla ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya maadili haki za binadamu, uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa.

Amesema jitihada za Serikali katika kuhakikisha uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla unakua haraka,  huenda zisifanikiwe kutokana na kukithiri kwa vitendo vya urasimu, vinavyodaiwa kufanywa na viongozi ama maofisa wa Serikali.

Vile vile Makalla amewataka wananchi kuisaidia Serikali kujenga misingi bora ya maadili kwenye jamii na watumishi wa umma kwa kuwafichua watendaji wasio waadilifu na wala rushwa.

Pia amesema endapo watatoa ushirikiano wa kutosha kwa taasisi mbalimbali za Serikali kwa kufichua vitendo vya ukiukwaji wa maadili unaofanywa na watumishi wa umma,jitihada za kukuza uchumi zitafanikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *