Bi. Theresa May ndiye mwanasiasa anayetarajiwa kuwa mrithi wa nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza inayoachwa rasmi leo na David Cameron.

Je, unayafahamu mambo makubwa mawili ambayo yanamsubiri Bi. May ayafanyie uamuzi wa haraka?

Tatizo la Uskochi

Ni dhahiri kuwa nchi ya Uskochi (Scotland) haikufurahishwa na matokeo ya kura ya maoni ambayo yalionyesha kuwa nchi ya Uingereza inataka kujiondoa kwenye muungano wa nchi za ulaya maarufu kama EU.

Ukweli huo unachagizwa na matokeo ya majimbo 32 ya Uskochi ambayo yote yalipiga kura ya kutaka Uingereza isalie EU.

Hili ni jukumu kubwa sana kwa Bi. May kuweza kulitatua kwa haraka kwasababu endapo misimamo miwili tofauti ndani ya nchi ya Uingereza italindwa na kila waziri mkuu, huenda kukatokea mgawanyiko mkubwa ambao utairudisha Uingereza nyuma.

Kujitoa EU

Ingawa Bi. May anatambulika kwa kupigia chapuo Uingereza kubaki kwenye muungano wa EU lakini ameshasisitiza kuwa KUJITOA kunamaanisha KUJITOA.

Bado haijafahamika iwapo kutakuwa na kura ya pili ya maoni au la kuhusu kuala la Uingereza kujitoa EU lakini hilo linaweza likachangiwa sana na ushawishi wa Bi. May pindi atakapotawazwa kuwa waziri mkuu wa pili mwanamke kwenye historia ya Uingereza.

HIVYO MAJUKUMU MAWILI MAKUBWA NI:

1: Kutatua suala la BREXIT

2: Kuiunganisha Uingereza

Theresa May: Waziri mkuu mtarajiwa wa Uingereza
Theresa May: Waziri mkuu mtarajiwa wa Uingereza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *