Bunge jana limepiga kura za kuwapitisha wawakilishi wa bunge la Afrika Mashariki ambapo wagombea saba pekee ndio waliopitishwa kwa kupigiwa kura za ndio.

Sita kati ya waliochaguliwa wanatoka Chama cha mapinduzi (CCM) na mmoja Chama cha wananchi CUF  huku wagombea wawili wa Chadema wakikosa sifa baada ya kupigiwa kura nyingi za Hapana.

Waliochaguliwa kwenye uchaguzi uliofanyika jana Bungeni mjini Dodoma ni kama wafuatao

  1. Fancy Nkuhi
    2. Happiness Legiko
    3. Maryam Ussi Yahya
    4. Dkt Abdullah Makame
    5. Dkt Ngwaru Maghembe
    6. Alhaj Adam Kimbisa

7.Habib Mnyaa (CUF)

Kutokana na matokeo hayo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekosa nafasi ya kupata mwakilishi kwenye Bunge la Afrika Mashariki.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *