Jumla ya watuhimiwa sita wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuktwa na pombe aina za viroba ambapo zimepigwa marufuku.

Watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti kufuatia msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Maafisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya DCP Dhahiri Kidavashari amewataja wafanyabiashara hao kuwa ni :-

  1. ERASMO DANDA Mfanyabiashara na Mkazi wa Ihanga Wilaya ya Mbarali ambaye alikamatwa akiwa na “viroba original” boksi 99 zenye thamani ya Tshs 9,768,000/= zikiwa zimehifadhiwa katika stoo yake.
  2. Mtuhumiwa mwingine aliyekamatwa ni JOYCE BATHLOMEO Mfanyabiashara na Mkazi wa Kibaoni Wilayani Chunya akiwa na viroba vya aina mbalimbali ambazo ni “high life”  paketi 180 na aina ya Fiesta paketi 450 zikiwa zinauzwa katika duka lake la jumla.
  3. Mtuhumiwa mwingine ni NESTORY FILBERTMfanyabiashara na mkazi wa Lupatingatinga Wilaya ya Chunya aliyekamatwa akiwa na viroba paketi 9,840 aina ya Shujaa na paketi 100 za Konyagi.
  4. FILBERT KALUMANZILA Mfanyabiashara na mkazi wa Makongolosi Wilaya ya Chunya akiwa na viroba paketi 240 aina ya ridder.
  5. JOSHUA MWAKAJA Mfanyabiashara na mkazi wa Makongolosi akiwa na viroba paketi 100 aina ya ridder na gun 165 na chupa za ridder 60.
  6. JACKSON ELIAS Mfanyabiashara na mkazi wa Makongolosi Wilaya ya Chunya akiwa na pombe kali paketi 225 aina mbalimbali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *