Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole ametangaza majina ya wagombea 12 watakaowania nafasi 6 za ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Akiyataja majina hayo mbele ya waandishi wa habari, Polepole amesema wagombea hao 12 wanane wanatoka Tanzania ambapo wanaume wanne na wanawake wanne na wagombea wanne wanatoka Zanzibar ambapo wanawake wawili na wanaume wawili.

Polepole amesema kuwa katika nafasi hizo sita, Tanzania Bara itatoa wabunge wanne, wanaume wawili na wanawake wawili na Zanzibar itatoa wabunge wawili ambapo mwaume mmoja na mwanamke mmoja.

Majina hayo yaliyotangazwa leo ni

Wanawake Tanzania Bara

 1. Zainabu Rashid Kawawa
 2. Happines Lugiko
 3. Happines Mgaula
 4. France Haji

Wanaume Tanzania Bara

 1. Mgwalu Jumanne Magembe
 2. Adam Kimbisa
 3. Anamringa Macha
 4. Makongoro Nyerere

Wanawake Zanzibar

 1. Mariam Ussi
 2. Rabia Hamid

Wanaume Zanzibar

 1. Abdalah Makame
 2. Mohamed Yusuf Nuh

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *