Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ametoa ratiba ya majeruhi wa shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha ambao walikuwa nchini Marekani kimatibabu kufuatia ajali walioipata.

Nyarandu kupitioa ukurasa wake wa instagram ameweka ratiba hiyo kuwa watapitia katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) ambapo mgeni rasmi atawasili saa mbili asubuhi.

RATIBA ya MAPOKEZI KIA: Familia na Wananchi wanatarajiwa KUWASILI KIA saa 3 asubuhi, Mgeni Rasmi atawasili saa 2 asubuhi, na Ndege aina ya DC-8 inayowaleta WATOTO itakua saa 3 asubuhi. Hafla itafanyika KIA, upande wa Magharibi mwa UWANJA kupitia VIP.

Pia ameandika kuwa  Wote mnakaribishwa! Kesho nitatoa RATIBA ya vile HAFLA ya uwanjani itakavyofanyika. (Mapema leo nilitembelea KIA kushiriki kupanga ITIFAKI na MPANGILIO wa HAFLA utakavyokuwa, na tayari nimempokea Daktari Bingwa Steve Meyer (akiwa na mke wake Dana Meyer) aliyeongoza matibabu ya WATOTO, sote tukiwa tayari kwa mapokezi.KARIBUNI sana!

Watoto hao Doreen Wilson na Sadia wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa hii Agosti 18, 2017 ambapo watapokelewa katika uwanja huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *