Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane ataendelea kuuguza jeraha lake la kifundo cha mguu wakati ambapo timu yake inakabiliana na CSKA Moscow katika kombe la klabu bingwa Ulaya leo usiku.

Harry Kane mwenye umri wa miaka 23 ameumia kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Sunderland ambapo Tottenham ilishinda 1-0 kwenye mechi hiyo.

Pia Tottenham itawakosa beki wake wa kushoto Danny Rose na viungo wa kati Eric Dier, Mousa Dembele na Moussa Sissoko.

Kwa upande mwingine kipa wa Leicester Kasper Schmeichel huenda akarudi kuichezea klabu yake katika mchuano wa kwanza wa kombe la vklabu bingwa Ulaya dhidi ya FC Porto kutoka Ureno.

Schmeichel amekuwa nje kwa mechi tatu tangu Leicester iifunge Cub Brugge katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi G kwenye michuano hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *