Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, P Funk A.K.A Majani  amemchana Master Jay baada ya kusema Harmorapa hana hana kipaji.

Majani ambaye ni mmiliki wa Bongo Records amemjia juu Master Jay kwa kumwambia kuwa hapaswi kuongelea habari za Harmorapa kwa kuwa mwanamuziki huyo ni Entertainer kwa hiyo ana haki ya kusaidiwa.

Wiki kadhaa zilizopita Master Jay alisema kuwa siku hizi wanamuziki wanapenda kiki lakini hakunua kitu wanachofanya na hawana kipaji akimtolea mfano Harmorapa.

P – Funk ameongeza kwa kusema kuwa Master Jay hatakiwi aongee kwa kuwa alikuwa akimletea wasanii wabovu na P funk kuwapotezea akitolea mfano wa msanii Ndugu Sulukuchu asiyejua hata kuongea kiswahili na John walker ambaye alikuwa ana kipaji cha kuigiza ulevi na sio kuimba.

Majani amemaliza kwa kusema kuwa  Harmorapa ni zaidi ya mwanamuziki kwani pia ni mburudishaji, na kusema hata Juma Nature alikuwa akipondwa alivyomchukua lakini akaja kuwa msanii mkubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *