Majambazi wamevamia mgahawa wa Dinners uliopo katika mtaa wa Kenyatta Road jijini Mwanza na kupora kiasi cha fedha kisichojulikana na kujeruhi watu wawili kwa risasi kabla ya kutoweka katika tukio hilo.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa majambazi hao wanadaiwa kuingia ndani ya mgahawa huo jana alasiri na kufyatua risasi kadhaa kutoka ndani ya mgahawa huo.

Tukio hio limetokea katika eneo ambalo limezungukwa na taasisi za kibenki ikiwemo benki ya NMB, Kenya Commercial Bank KCB na wakala wa benki ya CRDB na zote zikilindwa na askari ambao hawakuweza kutoa msaada wowote licha ya kuwa ndani ya mita 30 kutoka katika mgahawa huo.

Mmoja wa watu waliojeruhiwa alikuwa ni muuza mitumba nje ya mgahawa huo na mwingine akiwa na asili ya Asia ambaye haijajulikana alikuwa nani katika mgahawa huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema atazungumza na vyombo vya habari leo baada ya kupata taarifa kamili.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *