Majambazi wakiwa na silaha za moto, wamevamia duka moja lililopo Mtaa wa Nkurumah jiji la Mwanza na kumuua kwa kumpiga risasi mama mmoja mwenye asili ya Kihindi kisha kupora kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana bado.

Duka hilo linauza bidhaa mchanyanyiko Mini Supermarket pia hutoa huduma za miamala ya kifedha kwa njia ya mitandao ya simu za mkononi.

Imeelezwa kuwa wakati majambazi hao wakiwa kwenye harakati hizo, aliingia mama mmoja mwenye asili ya Kihindi kwa ajili ya kununua dawa za kutuliza maumivu, panadol, ndipo majambazi hao walipomfyatulia risasi tatu na kusababisha afariki dunia papo hapo kisha yenyewe kutoweka kusipojulikana.

Tukio hilo limetokea kwenye duka na matukio ya kuporwa kwa watoa huduma za miamala ya pesa kwa njia ya simu imekuwa sugu kwenye Jiji la Mwanza huku majambazi wakitekeleza uharifu huo kwa hutumia silaha za moto hivyo kuleta hofu na amani kutoweka miongoni mwa wakazi wa Mwanza.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *