Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwalinda watoto wa kike nchini.

Amesema hayo wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi anakopita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo.

Waziri mkuu amesema kuwa nia ya Serikali ni kupata watumishi ambao ni wataalamu wa kada tofauti kama madaktari, wanasheria, mafundi, walimu na hata Wakuu wa Wilaya ambao ni wanawake.

Pia Majaliwa amewaonya wazazi ambao huwa wanakubali kupewa fedha na wanaume waliowapa mimba mabinti zao na kuwaeleza kuwa kwa mujibu wa sheria ilivyo nao pia wanastahili kupewa adhabu ya kifungo jela.

Vile vile amemtaka ofisa wa elimu asimamie suala hilo kwa kuwahamisha baadhi ya walimu kutoka Ruangwa mjini na kuwapeleka shule za vijijini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *