Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk Frida Mokiti kubadilisha uongozi wa Kituo cha afya cha Levolosi baada ya kulalamikiwa na wananchi kuwa kinatoa huduma mbovu kwa wagonjwa.

Pia amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kujenga hospitali za wilaya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo jana wakati alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, ambako alisema tatizo la msongamano wa wagonjwa hospitali za rufaa na hospitali nyingine ni lazima lipatiwe ufunguzi.

Awali alipotembelea wodi ya akinamama wanaosubiri kujifungua, mmoja wa wagonjwa, Glory Paul anayeishi Olasiti jijini hapa alimweleza Waziri Mkuu kuwa mtoto wake alifia tumboni baada ya wauguzi na madaktari wa Kituo cha Afya cha Levolosi kuchelewa kumpatia matibabu.

kufanyiwa upasuaji wakanikatalia na kunilazimisha nijifungue kwa njia ya kawaida ambapo ilishindikana na baada ya muda waliniambia kuwa mtoto amekufa na wananifanyia upasuaji ili kuokoa maisha yangu,” alieleza Glory.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alisema amepokea maagizo ya Waziri Mkuu, Majaliwa, ambayo yanalenga kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *