Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Polisi kufanya upelelezi kuhusu miili iliyookotwa pembezoni mwa mto Ruvu wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali imepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kuokotwa kwa miili hiyo Desemba 8, mwaka huu na kueleza kuwa matukio kama hayo.

Majaliwa ametoa maagizo hayo katika Baraza la Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) lililofanyika kitaifa kijijini Shelui wilayani Iramba mkoani Singida.

Miili ya watu sita ilikutwa Desemba 7, mwaka huu kando ya mto Ruvu wilayani Bagamoyo ndani ya mifuko ya sandarusi na ikiwa imewekwa mawe ili isielee kisha mifuko hiyo kushonwa kama mzigo wa mazao na kutupwa mtoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *