Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana kuchunguza ni kwa nini Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonino Kilumbi amekwenda kutengeneza madawati kwa watu binafsi badala ya karakana ya Magereza kama ilivyokusudiwa na serikali.

Magereza Mkoa wa Dodoma ilipewa Sh milioni 24 na serikali ili kutengeneza madawati 480 na kila moja lilitakiwa kugharimu Sh 50,000.

Uongozi wa gereza hilo ulitengeneza madawati hayo kwa watu binafsi, ambapo dawa moja limegharimu Sh 70,000.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea Gereza la Isanga mkoani Dodoma akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo yanayotoa huduma za jamii mkoani humo.

Amesema kama gereza hilo halikuwa na uwezo wa kutengeneza madawati hayo kwanini kazi hiyo wasingeipeleka kwenye taasisi nyingine ya umma.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kilumbi amesema waliamua kupeleka kazi hiyo kwa watu binafsi kwa sababu hawana vifaa.

Waziri Mkuu alimtaka mkuu huyo wa magereza mkoa kuimarisha kitengo cha ufundi seremala na kuhakikisha anatumia vizuri nguvu kazi aliyonayo katika kuzalisha bidhaa mbalimbali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *