Winga wa Leicester City, Rihad Mahrez amesaini mkataba mpya wa miaka minne na mabingwa hao wa Uingereza ambapo mkataba huo utamuweka King Power mpaka msimu wa mwaka 2020.

Winga huyo alihusishwa kuihama timu hiyo baada ya baadhi ya klabu kutaka kumsaijili lakini sasa ameamua kubakia na kuisadia klabu hiyo kutetea taji lake la ligi kuu nchini Uingereza.

Mahrez ambaye ni raia wa Algeria alitakiwa na klabu ya Arsenal lakini ndoto ya klabu hiyo imeyeyuka baada ya winga huyo kusaini mkataba mpya mpaka msimu wa mwaka 2020.

marezi

Winga huyo aliachaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu nchini Uingereza msimu uliopita baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu na kuisadia timu yake kutwa taji la ligi kuu nchini Uingereza.

Leicester City imeanza ligi kwa kupoteza mchezo wa kwanza baada ya kufungwa 2-1 dhidi ya Hull City ugenini huku mechi ya pili wakitarajiwa kucheza dhidi ya Arsenal katika uwanja wa King Power siku ya Jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *