Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemzuia Msajili wa Vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi  kutoa fedha za ruzuku kwa Chama Cha Wananchi (CUF).

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano  ya Umma, CUF, Mbarala Maharagande imeeleza kwamba uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji  Wilfred Dyansobela.

Akitoa uamuzi huo Jaji Dyansobela amemtaka Msajili wa vyama vya siasa asitoe fedha za ruzuku mpaka hapo shauri namba 21/2017  dhidi ya msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)  litakaposikilizwa.

Shauri hilo linahusu fedha za ruzuku  Sh.milioni 369 ambazo zinadaiwa kutolewa kwa njia ya udanganyifu kwa chama hicho kwa upande wa Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba.

Katika shauri hilo Wakili Juma Nassor aliyekuwa anakitetea CUF aliwasilisha maombi hayo kwa  kusisitiza kuwa kwa mazingira yaliyopo ndani ya chama hicho ni vyema na busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kwa ruzuku kwenye chama hicho ziendelee kubaki serikalini

 Mawakili Nassor aliiomba  Mahakama Kuu kwamba uamuzi huo pia ufungamane na Kesi ya Msingi namba 23/2016 ya kuhoji maamuzi ya Msajili kumtambua Profesa Lipumba kwa nafasi ya Uenyekiti ambayo ipo mbele mbele ya Jaji Kihijo ambayo kwa sasa imekatiwa Rufa kwa maombi ya kufanyiwa marejeo mbele ya Mahakama ya Rufaa-Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *