Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeshindwa kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili video queen, Agnes Gerard ‘Masogange’ kwa sababu ana tatizo la kiafya.

Hayo yameelezwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya wakili wa Serikali Costantine Kakula kueleza shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Kwa upande wa wakili wa Masogange, Ruben Simwanza alimueleza Hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi hiyo ihairishwe.

Hakimu Mashauri aliharisha kesi hiyo hadi julai 25 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *