Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kuwa Agnes Gerald maarufu kama ‘Masogange’, anayo kesi ya kujibu kwa kudaiwa kutumia dawa za kulevya, hivyo anapaswa kujitetea.

Kesi hiyo ambayo imeunguruma leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, amesema kuwa amekubaliana na hoja za ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo mshtakiwa amekutwa na kesi ya kujibu na hivyo ana haki ya kujitetea.

Baada ya kauli ya hakimu huyo, Masogange amesema atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi watatu. Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu ambapo mtuhumiwa ataanza kujitetea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *