Mwanamuziki wa Marekani, Chris Brown amekatazwa kumuona mpenzi wake wa zamani, Karruche Tran baada ya kudai kwamba alitishia kumuua mwezi Disemba mwaka jana.

Karrueche Tran amepewa agizi hilo dhidi ya msanii huyo na mahakama akisema amemtishia kupitia jumbe tangu mwezi Disemba mwka jana.

Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 28 amemshutumu mwimbaji huyo kwa kumpiga tumboni na kumsukuma kwenye ngazi nyumbani lakini amesema kuwa hakuripoti kituo cha polisi.

Wawili hao walikuwa wapenzi mwaka 2015 lakini wakawachana baada ya miezi kadhaa kutokana na kutoelewana.

Uamuzi huo umetolewa na makahama kutokana na Chris Brown kumtishia mpenzi wake huyo wa zamani kuwa atamuua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *