Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi wa ama kupokea au kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya kwa sababu Hakimu hajamaliza kuandaa uamuzi huo.

Uamuzi huo ulitarajiwa utolewe leo October 4, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, lakini amesema bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi November 1, 2017.

Awali, Wakili wa Wema, Peter Kibatala aliiomba Mahakama isipokee hati hiyo kwa kuwa haikukidhi vigezo.

Mbali ya Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *