Mahakama ya katiba Katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo imeidhinisha ombi lililozusha mzozo la tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi wa Novemba ili orodha ya usajili wa wapiga kura iwekwe sawa.

Kiongozi wa mahakama ya katiba, Benoit Lwamba Bindu amesema mahakama hiyo inatambua kuwa kuna matatizo ya kiufundi na imeamrisha ‘kucheleweshwa kwa sababu zinazoeleweka.’

Imesema tume hiyo ni lazima ichapishe kalenda mpya ya uchaguzi wa urais ambao awali ulipangwa kufanyika Novemba 27.

Tume ya uchaguzi Congo iliwasilisha rufaa mahakamani ya kuchelewesha uchaguzi huo mnamo mwezi September.

Tume hiyo imesema huenda uchaguzi usiweze kuandaliwa hadi mwishoni mwa mwaka 2018, jambo linalozusha wasiwasi kuwa hofu na ghasia zitaongezeka.

Rais Joseph Kabila alitarajiwa kujiuzulu Desemba baada ya muda wake kikatiba kumalizika baada ya kuhudumu kwa mihula miwili madarakani.

Upinzani unasema kuwa Kabila anajaribu kuendelea kushikilia madaraka kwa kuchelewesha uchaguzi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *