Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder  Singh Sethi apewe matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili akiwa rumande.

Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Seth kudai anahitaji kuwa na nguvu ambayo haitopatikana kama Afya yake itakuwa dhaifu, hivyo ameomba apatiwe matibabu.

Kutokana na kuwa afya ni muhimu kwa binaadam, Mahakama imetoa kibali ili mshtakiwa huyo apate matibabu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 3 mwaka huu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa serikali, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *